Friday, March 15, 2019 China Itaandaa Siku ya Kusherehekea Mazingira kote Ulimwenguni Mwaka 2019 kuhusu Uchafuzi wa Hewa
Habari kwa vyombo vya habari

Nairobi, tarehe 15 Machi 2019 – Hivi leo, kiongozi wa uwakilishi wa China, Zhao Yingmin, naibu wa waziri wa mazingira na Joyce Msuya, kaimu wa kiongozi wa UN Environment walitangaza kwa pamoja kuwa nchi ya China itaandaa siku ya kusherehekea mazingira ulimwenguni tarehe 5 Juni, 2019 kuhusu uchafuzi wa hewa.

Takriban millioni 7 ya watu kote ulimwenguni huangamia mapema kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hewa, millioni 4 ya vifo hivi hufanyika Asia-Pacific.Siku ya nkusherehekea Mazingira kote ulimwenguni itahimiza serikali, viwanda, jamii na watu binafsi waje pamoja na kuchunguza nguvu zisizoisha na teknolojia za bustani za miche na kuboresha hewa katika mji na sehemu zote ulimwenguni.

Serikali ya China imejitolea kuandaa sherehe za siku ya mazingira katika miji kadhaa. Hangzhou katika wilaya ya Zhejiang itaandaa sherehe kuu.

Tangazo hili linakuja huku mawaziri wa mazingira kutoka kote ulimwenguni wakihudhuria mkutano wa kiwango cah juu Zaidi ulimwenguni kuhusu mazingira mjini Nairobi.Majadiliano katika mkutano wa nne wa UN Environment tarehe 11- 15 Machi yanataraajiwa kushughulikia masuala muhimu kama vile kumaliza uharibifu wa chakula na kuendeleza kusambaa kwa gari za kielektroniki.Inafuatia chapisho ya mapitio ya ripoti ya miaka 20 ya kudhibiti uchafuzi wa hewa Beijing.

“China itaandaa Sherehe za Siku Ya Mazingira Ulimwenguni 2019” Joyce Msuya alisema katika tangazo la Ijumaa.”Nchi hio imeonyesha uongozi mkubwa katika masuala yanayohusu uchafuzi wa hewa wa kinyumbani.Inaweza ikaelekeza dunia katika hatua kubwa.Uchafuzi wa hewa ni tatizo la dharura linalomkumba kila mtu.China sasa itakuwa inaongoza na kuanzisha hatua kote ulimwenguni ili kuokoa maisha.”

China ikiwa na sekta yake ya uzalishaji wa nguvu imeibuka kuongoza katika hali ya hewa.Nchi hii inamiliki nusu ya magari yanayotumia umeme kote ulimwenguni na asilimia 99 ikiwa ni basi za umeme.Serikali ya China, kupitia kuandaa Siku Ya Kusherehekea Mazingira 2019, itaweza kuonyesha uvumbuzi wake na maendeleo kuelekea mazingira safi.

Kulingana na ripoti mpya kuhusu uchafuzi wa hewa Asia na Pacific, utekelezaji wa sera 25 za kiteknolojia unaweza ukapunguza kaboni dioksidi kwa asilimia 20 na uzalishaji wa gesi ya metani kwa asilimia 45, ikipelekea thuluthi moja ya digrii ya Celsius ili kupunguza joto ulimwenguni.

Siku ya kusherehekea mazingira ulimwenguni ni sherehe inayoongozwa na UN Environment inayofanyika tarehe 5 Juni kila mwaka na inasherehekewa na maelfu ya jamii kote ulimwenguni.

Tangu ilipoanza katika mwaka wa 1972, imekua na kuwa sherehe kubwa ya kipekee ya mazingira yetu ya kila mwaka.

Ukweli kuhusu uchafuzi wa hewa:-

  • Asilimia 92 ya watu ulimwenguni hawapumui hewa safi
  • Uchafuzi wa hewa hugharimu dola trilioni 5 kila mwaka katika malipo ya ustawi
  • Uchafuzi wa ngazi ya chini ya ozoni inaweza ikapunguza mimea kuu kwa asilimia 26 kabla ya 2030.

MAELEZO KWA WAHARIRI

Kuhusu UN Environment:

UN Environment ni sauti ya mazingira inayoongoza.Inatoa programu za uongozi na inahimiza ushirikiano katika kulinda mazingira kupitia kuchochea, kujuza na kuwezesha mataifa na watu kuboresha maisha yao bila kuharibu maisha ya vizazi vijao. UN Environment inafanya kazi na serikali, sekta za kibinafsi, jamii na taasisi zingine za UN Na mashirika mengine ya kimataifa kote ulimwenguni.

Kwa habari zaidi, wasiliana nasi: UN Environment News & Media,  unenvironment-newsdesk[at]un.org

Recent Posts
Story Siku ya Mazingira Duniani ya Infosys – Kuondoa Kabisa Plastiki

Plastiki huwa karibu 90% ya takataka zote za bahari na vipande 46,000 vya plastiki vinavyofunika kila maili mraba. Ni wakati mzuri tunafaa kufahamu madhara yanayosababishwa na plastiki

Story Uendeshaji meli kwa kutumia plastiki mjini Amsterdam

Kiwanda kipya kinajengwa kwenye Bandari ya Amsterdam na kinatarajiwa kubadilisha utupaji taka ya plastiki. Kiwanda hiki kitatumia teknolojia mpya kuunda dizeli kwa kutumia plastiki ambayo awali haingeweza kutengenezwa upya po

}