Monday, July 9, 2018 Uendeshaji meli kwa kutumia plastiki mjini Amsterdam
Hadithi

Kiwanda kipya kinajengwa kwenye Bandari ya Amsterdam na kinatarajiwa kubadilisha utupaji taka ya plastiki. Kiwanda hiki kitatumia teknolojia mpya kuunda dizeli ya kuendesha meli za mizigo kwa kutumia plastiki ambayo awali haingeweza kutengenezwa upya.

Kiwanda hiki kinajengwa na kampuni ya Uholanzi ya Bin2Barrel iliyoanzishwa na wajasiriamali wa kudhibiti taka, Floris Geeris na Paul Harkema mwaka wa 2012. Japo teknolojia ya kutengeneza bidhaa upya kwa kutumia kemikali imewahi kutumika awali, Bin2Barrel ndiyo kampuni ya kwanza kuitumia kibiashara.

Kutokana na ushirikiano na Bandari ya Amsterdam na hiba iliyotolewa na serikali ya Uholanzi, kiwanda hiki kinatarajiwa kuanza kuendesha shughuli zake kufikia mwishoni mwa 2018. Kila kitu kikiwa shwari, hiki ndicho kitakuwa cha kwanza kati ya viwanda vinne vya ‘fueli kutoka kwa plastiki’ kujengwa karibu na bandari. Katika mwaka wa kwanza inakadiriwa kuwa tani 35,000 za

taka zitatumika kuzalisha lita milioni 30 za fueli, hivyo kutumia taka ambayo kama sivyo ingetupwa.

Mradi huu una manufaa mengi kwa mazingira kwenye mchakato mzima wa kuongeza thamani. Bandari ya Amsterdam inakadiria kuwa viwango vya CO2 vinavyotolewa vitapungua kwa tani 57,000 kila mwaka.

image
Picha imepigwa na Pixabay

Faida kuu zaidi ni katika utupaji taka. Plastiki inayotumiwa viwandani haiwezi kutengenezwa upya na kufikia sasa, plastiki hii huchomwa au hutupwa. Kwa

kuibadilisha kuwa fueli, plastiki inatumika upya na haifiki kwenye mazingira kama taka.

Faida nyingine kuu ni fueli inayoundwa kwenye kiwanda hiki, ambayo inauzwa kwenye sekta ya bahari. Dizeli ya kawaida inahitaji kiwango kikubwa cha nishati kuchimbuliwa, kusafirishwa na hatimaye kutumiwa. Kwa sababu haitumii mchakato wa kawaida wa utengenezaji, viwango vya CO2 vinavyotolewa na dizeli inayoundwa na kiwanda cha Bin2Barrel vitapungua kwa asilimia 80. Pia inatoa mbadala kwa nishati ya kiasili, ambayo huhitaji kiasi kikubwa cha ardhi na rasilimali kuzalisha.

Wakosoaji wa utumiaji taka kuzalisha nishati wanadai kuwa aina hii ya teknolojia inalemaza ukuaji wa nishati mbadala, kama vile jua na upepo. Hata hivyo, wanaopendekeza teknolojia hii ya utengenezaji upya wanadai kuwa viwanda kama hivi ni muhimu, kwa sababu vinazalisha nishati kwa kutumia mbinu bora zaidi zisizoathiri mazingira ikilinganishwa na viwanda vinavyotumia nishati mbadala na pia vinashughulikia suala linalokithiri la uchafuzi wa plastiki.

image
Picha imepigwa na Pixabay

Roon van Maanen, Mkuu wa Idara ya Nishati Mbadala na Utengenezaji Upya kwenye Bandari ya Amsterdam, alieleza umuhimu wa kiwanda hiki. “Utumiaji wa na mbinu zisizofaa za kutengeneza plastiki husababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kote ulimwenguni. Bin2Barrel imezindua teknolojia bunifu na inayohitajika haraka itakayotuwezesha kujinufaisha kutokana na taka ambayo kwa sasa ni ya kutupwa. Kwa kuunda bidhaa mpya kwa kutumia taka, kiwanda hiki kitaisaidia Bandari kutumia uchumi wa kimviringo.”

Ni wazi kuwa ili kuhakikisha tunahifadhi rasilimali, tunahitaji kusitisha kutumia nishati mbadala. Waanzilishi wa Bin2Barrel wanakubali hili na kwa mujibu wao, ‘utumiaji plastiki kuzalisha nishati’ ni hatua muhimu kwa sasa. Lengo la kampuni si kuwa kiwanda kikubwa zaidi kinachotengeneza fueli, bali ni kutumia plastiki upya na kuunga mkono uchumi wa kimviringo. Lengo kuu la kampuni ni “utumiaji kemikali kuunda bidhaa upya, ili kuweza kutengeneza plastiki mpya.” Teknolojia itakapokuwa ya hali ya juu zaidi Bin2Barrel ingependa kujihusisha katika kutumia taka ya plastiki kuunda elementi muhimu za kemikali, zinazoweza kutumiwa upya kuunda bidhaa mpya

Recent Posts
Story Siku ya Mazingira Duniani ya Infosys – Kuondoa Kabisa Plastiki

Plastiki huwa karibu 90% ya takataka zote za bahari na vipande 46,000 vya plastiki vinavyofunika kila maili mraba. Ni wakati mzuri tunafaa kufahamu madhara yanayosababishwa na plastiki

Press Release China Itaandaa Siku ya Kusherehekea Mazingira kote Ulimwenguni Mwaka 2019 kuhusu Uchafuzi wa Hewa

 Nairobi, 15 March 2019 – Today, the head of Chinese delegation, Zhao Yingmin, Vice Minister of Ecology and Environment, and Joyce Msuya, Acting Head of UN Environment, jointly announced that China will host the global World Environment Day celebrations on 5 June 2019 with a theme of air pollution.

}